Mungu amesema, “Mimi ndimi BWANA Mungu wako aliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu cho chote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji.
” (Kutoka 20:2-4).
Kazi ya shetani ndiyo kupotosha tabia ya Mungu mawazoni mwetu; kazi ya shetani ndiyo kuharibu sura ya kweli ya Mungu mioyoni mwetu ili tusiamini Mungu, ili tusiamini wema, neema na rehema zake, ili tusiamini Yesu anaweza kutuokoa kabisa!
Kwanza Ibilisi ankuja kutuvuta tufanye dhambi. Mara alipofaulu kufanya hivyo, anaanza kutushitaki kwa kali, kutulaumu na kuponda dhamira yetu ili tujisikie hatufai kabisa na tumekataliwa kabisa!
Mwanzoni shetani alikuja bustani akamdanganya Eva, akamvuta afanye dhambi. Shetani anakuja na anaongea na maneno kama haya mioyoni mwetu, “Inaonekana tamu sana, siyo ndiyo? Unapenda hiyo, siyo ndiyo? Unahitaji hiyo, siyo ndiyo? Jambo hili litakuletea furaha, raha na anasa! Inavuta sana, siyo nidyo? Huwezi kupinga! Chukue tu! Fanya tu! Hutapata hasara!” Mawazo haya yote ni udanganyifu tu! Shetani anataka ufanye dhambi tu! Mawazo haya siyo mawazo yako tu. Shetani mwenyewe aliyaingiza mawazo hayo moyoni mwako ili uamini uongo wake na usiamini Mungu!
Mara Adamu na Eva walipofanya dhambi, walianguka gizani kabisa na mara moja shetani aliendelea kazi yake kwa kupotosha tabia ya Mungu mioyoni mwao! Adamu na Eva walijificha mara moja! Kwa nini? Kwa sababu walifikiri Mungu atakapokuja, atawahukumu, kuwaponda na kuwaharibu! Walifikiri kwamba sasa Mungu hawapendi na Yeye ndiye kinyume chao na dhidi yao. Walitetemeka kwa hofu! Mawazo haya siyo toba mioyoni mwao! Mawazo hayo yanatokana na shetani! Mawazo haya ni matokeo ya kupokea maongo (sumu) ya shetani anayepotosha sura ya Mungu ili tufikiri Mungu ndiye dhidi yetu!
Adamu na Eva waliweza kufikiri na kusema, “Kumbe, tulikosa kabisa, tulifanya dhambi mbele ya Mungu. Kwa kweli Mungu alifanya yote vizuri na alitubariki kupita kiasi na yule nyoka alitudanganya! Haya, na twende kwake Mungu na tukiri dhambi zetu mbele Yake. Na tuiname mbele Yake na tutobe! Mungu ni Mwema na Mwenye huruma, inawezekana atatusamehe!”
Haya ni toba! Waliweza kufanya hivyo – lakini sumu (uongo) ya shetani ambayo inapotosha tabia (sura) ya Mungu machoni pa watu iliingia sana mioyoni mwa Adamu na Eva na iliwaongoza kutokumwamini Mungu na kuamini Mungu ni kinyume chao! Hiyo nidyo kazi ya shetani. Hilo ndilo lengo lake – tufikiri Mungu hatupendi; kufikiri Mungu ni dhidi yetu; kufikiri Mungu atatuponda na kutuharibu! Ibilisi anataka kuharibu imani yetu kwake Yesu na kutuweka gizani ambopo hatuamini Mungu. Tukiendelea kuamini Mungu ni kinyume chetu, ndipo hatutaweza kupokea msaada kutoka Mungu (ila Yeye ni juu yote na anaweza kufanya apendalo) kwa sababu tupo hali ya kutokuamini! Kwa sababu hiyo, watu wa Israeli walizunguka jangwani miaka arobaini!
Kwa nini nilinukulu Kutoaka 20:2-4 hapo juu? Kwa sababu Mungu amejidhihirisha ifuatayo:
“BWANA, BWANA, Mungu MWENYE HURUMA na NEEMA, ASIYE MWEPESI WA HASIRA, MWINGI wa upendo na uaminifu…” (Kutoka 34:6).
Hiyo ndiyo tabia au ‘sura’ ya Mungu, lakini shetani anataka kuchora ‘sanamu’ mawazoni au moyoni mwako; anajaribu kubadilisha ‘sura’ ya Mungu afanye Mungu ni kama mtu mkali machoni pako kama Mungu ndiye mbali nawe anayetaka kukuharibu! Hiyo ni kazi ya Ibilisi kila siku! Kwa hiyo Biblia inasema, “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu Zake. Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za Shetani.” (Waefeso 6:10,11).
Kama nilivyosema, kwanza Ibilisi anakuja kutuvuta na kutushawishi tufanye dhambi. Lakini mara tunapokosa, anabadilisha mbinu yake na anaanza kwa nguvu kutulaumu, “Onaona, hufai! Hufai kabisa! Unakosa tena! Hupendi Mungu kwa kweli. Mungu hakupendi! Ulikosa mara nyingi. Huwezi kushinda dhambi hiyo! Huna uwezo kushinda! Wewe ni mwenye udhaifu! Utashindwa tu! Wewe si kitu! Wengine wanashinda na wanabarikiwa lakini siyo wewe kwa sababu Mungu siyo kwa upande wako!” Kwa maneno na mawazo haya shetani anataka kutukata tamaa kabisa ili tusiamini Mungu, ili tusiende kwake Yesu mara moja tupate rehema na msamaha! Nataka kusema maneno au mawazo hayo siyo mawazo yako! Kwa msingi yanatokana na shetani! Maneno haya ni sauti yake! Kwa nini naweza kusema hayo? Kwa sababu mimi najua, na wewe pia unajua, mawazo kama hayo yanatuvuta na kutusukumu MBALI na uwepo ya Bwana ili tujisikie peke yetu, bila matumaini! Siyo ndiyo ndugu na dada? Naamini unajua ninayoyandika ni kweli.
Hali hiyo ambayo niliandika juu yake hapo juu siyo hali ya toba! Ni hali ya kutokuamini Mungu na inatuongoza mbali na Bwana Yesu katiak maisha ya kiroho yetu. Sasa, huduma ya Roho Mtakatifu ni tofauti sana na kazi ya Ibilisi! Kama tukikosa au tukishindwa, Roho ya Mungu anaongea kwa sauti ya pole sana kwa dhamira yetu! Biblia inasema Roho ya Mungu ni kama HUA. Siyo kama mtu mkubwa mkali ambaye anakuja kutupiga na fimbo! Bwana apewe sifa kwa neema Yake! Roho hatupondi, hatusukumu au kutufukuza mbali na Mungu! Roho ya Mungu anatujulisha kosa letu lakini pamoja na hiyo anatuonyesha Yesu ndiye Mwokozi na Msaada wetu, yaani, kwa huduma Yake, Roho ya Mungu anatuvuta tuje kwa Bwana, na tuje mara moja! Unaona, huduma na mawazo ya shetani yanakusukuma na kufukuza mbali na Bwana, na kinyume chake, huduma na sauti ya Roho ya Mungu inakuvuta kwa Bwana upate msamaha, rehema na neema ya Mungu mara moja! Bwana asifiwe kwa neema kama hiyo kuu! Na hiyo siyo kwamba tufanye dhambi tena lakini tupate faraja na neema ili tumwamini Mungu tushinde kwa neema ya Bwana na kwa nguvu za Roho Yake! Usikate tamaa! Kila mara nenda kwa Bwana; mwamini Yeye kwa moyo wako wote; soma neno lake; chukua muda uwe pamoja na Baba na Mwana; mpende Bwana kwa moyo wako wote na ujitoe kwake kabisa kila siku. Usikatae tamaa. Endelee na Bwana zaidi kuliko wakati uliopita na Mungu akubariki!
Najua siku moja wote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, lakini niliandika mambo haya ili sisi sote tuweze kusimama mbele ya Bwana siku ile kwa furaha na siyo kwa huzuni!
Pia lazima niseme ninaongea juu ya “dhambi inayotuzinga kwa urahisi” – Waebr.12:1 – ambayo neno la Mungu anatuambia “tuweke kando”. Siongei juu ya uzinzi na uasherati! Ukifanya hivyo, lazima utobe na uokoke kwanza! Pia sio lengo langu kumpa ye yote sababu au kisingizio afanye dhambi! Ninaandika jumbe hiyo kwa ajili ya wakristo wa kweli kwa sababu napenda kuwatia moyo katika Bwana kwa sababu najua shetani anatumia ubinu hizo ili tusiendeleeni mbele katika wokovu wa Yesu Kristo; anataka kutukata tamaa kabisa ili tuache tumaini la kushinda! Anataka tukae chini na kulalamika hali yetu, kutupa mavumbi juu ya kichwa chetu, kujihurumia sisi wenyewe kana kwamba hauna msaada na tupo peke yetu! Na anataka tudumu katika hali hiyo hiyo sikuzote mpaka mwisho kana kwamba hatuwezi kushinda na kana kwamba Mungu ni dhidi yetu au alituacha! Lakini neno la Mungu lisemalo?
“AMKA, amka, Ee Sayuni, JIVIKE nguvu. Vaa mavazi yako ya fahari, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu. Jikung’ute mavumbi yako, INUKA, uketi kwenye kiti cha enzi, Ee Yerusalemu. JIFUNGUE minyororo iliyo shingoni mwako. Ee Binti Sayuni uliye mateka.” (Isaya 52:1, 2)
“Mimi, naam MIMI, NDIMI NIWAFARIJIE NINYI. Ninyi ni nani hata kuwaogopa wanadamu wanaokufa, wana wa wanadamu ambao ni majani tu, kwamba mnamsahau BWANA Muumba wenu, aliyezitanda mbingu na kuiweka misingi ya dunia, kwamba mnaishi katika hofu siku zote kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu, ambaye nia yake ni kuangamiza? IKO WAPI BASI GHADHABU YA MDHALIMU?” (Isaya 51:12,13).
“Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako itakayofanikiwa nawe utauthibitisha kuwa mwongo kila ulimi utakaokushtaki. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu, asema BWANA”. (Isaya 54:17).
“Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja Naye?” (Warumi 8:32).
“Lakini MUNGU ANAUDHIHIRISHA UPENDO WAKE KWETU kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa damu Yake, SI ZAIDI SANA TUTAOKOLEWA KUTOKA KATIKA GHADHABU kwa Yeye! Kwa kuwa kama tulipokuwa adui wa Mungu tulipatanishwa naye kwa njia ya kifo cha Mwanawe, SI ZAIDI SANA TUKIISHA KUPATANISHWA, TUTAOKOLEWA KWA UZIMA WAKE.” (Warumi 5:9,10).
NJIA MBILI
“Kwa sababu walipomjua Mungu, hawakumtukuza Yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.” (Warumi 1:21).
Tukisoma mstari huu tunaona kwamba kwetu tumjuao Mungu, ni lazima tuchague kati ya mambo mawili katika maisha yetu ya kila siku: kutambua tabia ya Mungu na kwa hiyo kumtukuza Mungu na kumshukuru kwa kuwa Yeye ndiye Mungu, AU kutekwa nyara na mawazo yanayopinga wema na upendo wa Mungu. Fikira hizi hujaribu kujionyesha kuwa kweli tukiangalia mazingira yetu, lakini ni kutokuamini tu! Kwa mfano fikira za kukataliwa. Mawazo haya yanatuongoza gizani na hapo tunatumikia mambo mabaya mengine kama wivu, husuda, uchungu, chuki nkd.
Kwa hiyo Mungu aliwaambia Waisraeli,
“Kwa sababu hukumtumikia BWANA Mungu wako kwa furaha na kwa moyo wa kushukuru kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote; kwa hiyo utawatumikia adui zako…” (Kumbu.28:47,48).
Adui zetu ni kutokuamini, chuki, wivu, hasira, uchungu, kujihurumia, wasiwasi, fitina, majivuno, uchafu nkd.
Kumshukuru Mungu siyo jambo la kinywa tu! Lazima sifa na shukrani zetu kwa Mungu zinatokana na mioyo yetu! Kwa haraka utatambua kwamba kumsifu na kumtukuza Bwana moyoni mwako siyo jambo ambalo linaunga mkono kutokuamini, kujihurumia, kulalamika, uchungu au wivu! Mambo haya hayawezi kuishi pamoja wakati ule ule moyoni mwetu! Kumshukuru na kumsifu Bwana kweli kweli ni lazima kupinga, kushinda na kuacha kila wazo la kutokuamini! Jambo hili hugusa mioyo yetu kwa ndani sana, kwa hiyo Paulo anatufundisha,
“Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo…” (2 Wakor.10:4,5).
Anaongea juu ya ‘ngome’ ya kutokuamini. Usitekwe nyara na mawazo ya giza na batili, kama kujihurumia na kukataliwa. Tembee kwa nguvu za Bwana na ushinde kila wazo lililoinuka dhidi ya kumjua Mungu ili tumtii Kristo Yesu katika kila jambo. Na tumtumikie Mungu kwa furaha na kumtukuza Yeye katika mawazo yetu. Tukifanya hivyo, tutabarikiwa kupita kiasi na tutamtukuza Bwana Yesu
Post a Comment