Enjoy High Desert Design
Situated just one block from the beach in Venice, California, this award-winning local landmark epitomizes modernist cool.
Situated just one block from the beach in Venice, California, this award-winning local landmark epitomizes modernist cool.
Situated just one block from the beach in Venice, California, this award-winning local landmark epitomizes modernist cool.
Situated just one block from the beach in Venice, California, this award-winning local landmark epitomizes modernist cool.
Msifadhaike mioyoni mwenu. Mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. Kama sivyo, ningaliwaambia, maana naenda kuwaandalia mahali. Basi, mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. (Yohana 14:1-3. Maneno mepesi kukazia).Kilicho wazi katika maneno ya Yesu ni uwezekano wa kurudi Kwake wakati wale mitume wakiwa bado hai. Ukweli ni kwamba, baada ya kusikia maneno ya Yesu, wangeweza kudhani tu kwamba atarudi kuwachukua wakiwa bado hai.
Kwa hiyo ndugu, vumilieni hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani. Huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia (Yakobo 5:7, 8. Maneno mepesi kukazia).Yakobo asingekuwa na haja ya kuwashauri wasomaji wake kuvumilia kuhusu kitu ambacho kisingetokea maishani mwao. Yeye aliamini kwamba kuja kwa Bwana “kunakaribia.” Kimantiki, Yakobo aliandika barua yake wakati kanisa lilipokuwa linapitia mateso makali (ona Yakobo 1:2-4), wakati ambapo waamini wangetamani sana kurudi kwa Bwana wao.
Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo (1Wathes. 4:13-18. Maneno mepesi kukazia).[1]Kutokana na hayo tunajifunza pia kwamba wakati Yesu atakaporudi kutoka mbinguni, miili ya waamini waliokufa itafufuliwa, kisha, pamoja na waamini walio hai wakati wa kuja Kwake, “kunyakuliwa ili kumlaki Bwana hewani” (Unyakuo). Kwa kuwa Paulo naye alitaja kwamba Yesu angewaleta wale waliokufa “ndani Yake” kutoka mbinguni, tunachoweza kusema ni kwamba wakati wa Unyakuo, roho za waamini walioko mbinguni zitaunganishwa na miili yao iliyofufuliwa punde tu.
Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. …Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia,basi iweni na akili, mkeshe katika sala. … Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe (1Petro 1:13; 4:7, 13. Maneno mepesi kukazia).[2]Na Yohana naye, alipoandika barua zake kwa makanisa, aliamini kwamba mwisho ulikuwa karibu, na kwamba wasomaji wa siku zake wangeona kurudi kwa Yesu.
Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. … Na sasa watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake. … Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu (1Yohana 2:18, 28; 3:2, 3. Maneno mepesi kukazia).
Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika sikuza mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, ‘Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.’ Maana hufumba macho yao wasione neno hili yakuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji kwa neno la Mungu. Kwa hayo dunia ile ya wakati ule ioligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. Lakini wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea” (2Petro 3:3-10).Petro anathibitisha kwamba kukawia kurudi kwa Yesu ni kwa sababu ya upendo na rehema na huruma Zake – anataka kutoa nafasi zaidi watu watubu. Lakini anasema pia kwamba hakuna mashaka yoyote – Yesu atarudi. Na atakaporudi, atakuja akiwa na ghadhabu kubwa.
Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni. Wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. Naye akajibu akawaambia, ‘Hamyaoni haya yote? Amin nawaambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.’Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha wakisema, ‘Tuambie! Mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?’ (Mathayo 24:1-3).Wanafunzi wa Yesu walitaka kujua habari za wakati ujao. Sana sana walitaka kujua majengo ya hekalu yangebomolewa lini (kama Yesu alivyokuwa ametabiri) na ishara gani ingeonyesha wakati wa kurudi Kwake na mwisho wa wakati.
Yesu akajibu akawaambia, ‘Angalieni mtu asiwadanganye [ninyi]. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni [ninyi] msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifal na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.’ (Mathayo 24:4-8. Maneno mepesi kukazia).Kutokana na jinsi mahubiri hayo yalivyoanza, ni dhahiri kwamba Yesu aliamini kwamba hao wanafunzi Wake wa karne ya kwanza wangekuwa hai wakati ishara hizo zinazotangulia kurudi Kwake zinapotendeka. Ona anasema nao moja kwa moja, kibinafsi. Katika sura hii ya 24, Yesu anasema na wanafunzi Wkae moja kw amoja zaidi ya mara ishirini. Basi, wasikilizaji Wake wote wangeamini kwamba wataishi na kuona hayo yote ambayo Yesu ametabiri.
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukuwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja (Mathayo 24:9-14. Maneno mepesikukazia).Hapa tena – kama ungewauliza wale waliomsikiliza Yesu siku hiyo swali hili: “Je, mnatazamia kuwa hai ili kuona kutimia kwa mambo hayo?” bila shaka wangejibu ndiyo kwa uhakika sana, maana Yesu alisema nao moja kwa moja.
Na kutakuwa wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele (Danieli 12:1, 2).Wokovu bado utatolewa kwa neema hata katika siku hizo, maana Yesu aliahidi kwamba Injili itahubiriwa kwa mataifa yote, kutoa nafasi moja ya mwisho ya kutubu, ndipo mwisho utakapokuja.[4] Tunasoma kitu katika Kitabu cha Ufunuo ambacho kinaweza kuwa kutimizwa kwa ahadi ya Yesu.
Kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injli ya milele, awahubirihao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa. Akasema kwa sauti kuu, ‘Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji’. (Ufunuo 14:6, 7. Maneno mepesikukazia).Kuna wanaodhani kwamba sababu ya malaika kuhubiri Injili wakati huo ni kwamba, kufikia hapo katika kipindi cha dhiki ya miaka saba, Unyakuo utakuwa umetokea na waamini wote watakuwa wameondoka. Lakini, hayo ni mawazo tu.
Basi, hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; wala aliye shambani asirudi nyuma kuchukua nguo yake. Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.[5] Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo (Mathayo 24:15-22).Hayo ni maelezo yaliyo dhahiri zaidi kuhusu dhiki ambayo Yesu alizungumzia mapema (ktk 24:9). Wakati mpingakristo atakapotangaza kwamba yeye ni Mungu kutoka hekalu la Yerusalemu, mateso yasiyofikirika yatatokea dhidi ya wanaomwamini Yesu. Kwa kujitangaza kwamba yeye ni Mungu, mpingakristo atatazamia kilamtu kutambua uungu wake. Basi, wafuasi wote wa kweli wa Kristo watakuwa maadui wa taifa, watu wa kusakwa na kuuawa. Ndiyo sababu Yesu aliwaambia waamini wa Uyahudi wakimbilie milimani bila kukawia, wakiomba kwamba kutoroka kwao kusizuiwe na sababu yoyote ile.
Naye [mpingakristo] akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa (Ufunuo 13:5-7. Maneno mepesi kukazia).Ona hapo kwamba mpingakristo atapewa “uwezo wa kufanya kazi yake” kwa miezi arobaini na mbili, au, miaka mitatu na nusu kamili. Huu ndiyo wakati unaoitwa nusu ya wakati wa kipindi cha Dhiki ya miaka saba. Ni sawa kabisa kufikiri kwamba ni ile miezi arobaini na mbili ya mwisho ya Dhiki, ndipo mpingakristo atakapopewa “uwezo wa kufanya kazi yake,” kwa sababu mamlaka yake yataondolewa kabisa wakati Kristo atakaporudi kufanya vita naye na majeshi yake wakati wa kumalizika kwa Dhiki.
Nikatazama, na pembe iyo hiyo [mpingakristo] ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; hata akaja huyo mzee wa siku [Mungu], nao watakatifu wake Aliye Juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme. … Naye [mpingakristo] atanena maneno kinyume chake Aliye Juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye Juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati (Danieli 7:21, 22; 25. Maneno mepesi kukazia).Danieli alitabiri kwamba watakatifu wangetiwa mikononi mwa mpingakristo kwa “wakati, nyakati, na nusu wakati.” Maneno hayo yaeleweke kwamba ni miaka mitatu na nusu, kama utafananisha na Ufunuo 12:6 na 14. Tunaambiwa katika Ufunuo 12:6 kwamba mwanamke fulani ambaye ni mfano, atapewa mahali pa kujificha nyikani ili “atunzwe na kulishwa” huko kwa muda wa siku 1,260, ambazo ni sawa na miaka mitatu na nusu kwa mwaka wenye siku 360. Kisha, mistari nane baadaye, anatajwa tena, na wakati huo inasemekana atapewa mahali nyikani ili “atunzwe na kulishwa” kwa “wakati, nyakati, na nusu ya wakati.” Basi, “wakati, nyakati, na nusu ya wakati” ni sawa na zile siku 1,260, au miaka mitatu na nusu.
Wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa popote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai (Mathayo 24:23-28).Ona tena hapa jinsi Yesu anavyosema na wanafunzi moja kwa moja. Wasikilizaji Wake pale Mlima wa Mizeituni wangetazamia kuishi mpaka waone kutokea kwa makristo wa uongo na manabii wa uongo ambao wangetenda miujiza mikubwa. Na bila shaka wangetazamia kumwona Yesu akirudi mawinguni kama umeme.
Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika, ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu (Mathayo 24:29-31).Mifano au picha katika sehemu hii ya mafundisho ya Yesu pale Mlima wa Mizeituni bila shaka ingekuwa inafahamika na Wayahudi wa siku Zake, maana inatoka katika Isaya na Yoeli, na inazungumzia hukumu ya mwisho ya Mungu, mwisho wa dunia. Mara nyingi huitwa “siku ya Bwana”, wakati jua na mwzi vitatiwa giza (ona Isaya 13:10, 11; Yoeli 2:31). Ndipo wakazi wote wa dunia watakapomwona Yesu akirudi mawinguni katika utukufu Wake, nao wataomboleza. Kisha malaika wa Yesu “watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu,” kuonyesha kwamba waamini watanyakuliwa na kukusanywa ili kumlaki Yesu mawinguni, na hayo yote yatatokea baada ya mlio wa “baragumu”.
Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tuli hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. Lakini ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani n salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa (1Wathes. 4:13 – 5:3. Maneno mepesi kukazia).Paulo aliandika juu ya Yesu kuja kutoka mbinguni kwa parapanda ya Mungu na kwamba waamini watanyakuliwa “mawinguni ili kumlaki Bwana hewani.” Ni sawa kabisa na yale Yesu aliyokuwa akieleza katika Mathayo 24:30, 31 – yanayotokea baada ya kutokea kwa mpingakristo na dhiki.
Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbingunipamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu,na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maagamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakaifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu). (2Wathes. 1:6-10. Maneno mepesi kukazia)Paulo alisema kwamba wakati ambao Yesu angerudi kuwapa nafuu Wathesalonike waliokuwa wanateswa (ona 1Wathes. 1:4, 5), angetokea “pamoja na malaika wake katika mwali wa moto” ili kuwaadhibu wale waliokuwa wanawatesa wao, kutoa hukumu ya haki, inayostahili. Hii haifanani na kile kinachosemwa na wengi, kwamba Unyakuo utatokea kabla ya dhiki, na kanisa kunyakuliwa na Kristo kabla ya kile kipindi cha dhiki cha miaka saba kuanza. Hii pia huitwa kuja kwa siri kwa Yesu ili kunyakua kanisa Lake. Hapana kabisa! Maelezo haya yanafanana na kile ambacho Yesu alieleza katika Mathayo 24:30, 31 – kurudi Kwake karibu aumwishoni mwa kipindi cha dhiki kuu – anapowanyakua waaminio na kumimina hasira Yake juu ya wasoiamini.
Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo (2Wathes. 2:1, 2).Kwanza: Ona kwamba mada ya Paulo ni kurudi kwa Kristo na Unyakuo. Aliandika kuhusu “kukusanyika kwetu mbele zake,” akitumia maneno yale yale ambayo Yesu alitumia katika Mathayo 24:31, alipozungumza juu ya malaika ambao “wangekusanya” wateule Wake “kutoka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho ule.”
Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu (2Wathes. 2:3, 4. Maneno mepesikukazia).Wakristo Wathesalonike walikuwa wanadanganywa kwa namna fulani kwamba siku ya bwana – ambayo kulingana na Paulo lazima ianze kwa Unyakuo na kurudi kwa Kristo – ilikuwa imekwisha fika. Akatamka wazi wazi kwamba haiji mpaka baada ya ule ukengeufu (labda ndiyo kule kurudi nyuma ambako Yesu alizungumzia katika Mathayo 24:10) na baada ya mpingakristo kujitangaza kwamba ni Mungu kutoka hekalu la Yerusalemu. Basi, Paulo anawaambia waamini Wathesalonike wazi wazi kwamba wasitazamie kurudi kwa Kristo – au Unyakuo – wala siku ya Bwana, mpaka baada ya tamko la mpingakristo kwamba ni Mungu.[6]
Je, hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa (2Wathes. 2:5-10).Paulo alitamka kwamba mpingakristo atakomeshwa “kwa ufunuo wa kuja Kwake” Kristo. Kama “ufunuo” Wake ni sawa na ule unaotajwa wakati wa Unyakuo – kiasi cha mistari tisa nyuma (ktk 2:1), basi mpingakristo atauawa wakati huo huo ambapo Kanisa litakusanywa ili kumlaki Bwana hewani. Hii inalingana na taarifa itolewayo katika Ufunuo sura ya 19 na 20. Hapo tunasoma juu ya kurudi kwa Kristo (ona Ufunuo 19:11-16), kuangamizwa kwa mpingakristo na majeshi yake (ona 19:17-21), kufungwa kwa Shetani (ona 20:1-3) na “ufufuo wa kwanza” (ona 20:4-6), ambapo waamini waliouawa katika kipindi cha Dhiki yamiaka saba watafufuliwa. Kama huu ndiyo ufufuo wa kwanza kweli kweli kwa maana ya jumla kwamba ni kwa ajili ya wenye haki, basi hakuna mashaka kwamba Unyakuo na kurudi kwa Kristo katika hasira Yake kunatokea wakati huo huo ambapo mpingakristo anaharibiwa, maana, Maandiko yanatuambia wazi kabisa kwamba wote waliokufa katika Kristo watafufuliwa wakati wa Unyakuo (ona 1Wathes. 4:15-17).[7]
Basi kwa mtini jifunzeni mfano. Tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu. Nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. Amin nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.[8]Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe (Mathayo 24:32-35).Yesu hakutaka wanafunzi Wake wanaswe bila kufahamu – na hilo ndilo jambo la msingi katika Mafundisho ya pale Mlima wa Mizeituni. Wangejua kwamba “yuko malangoni” baada ya kuona “mambo hayo yote” – dhiki duniani kote, kurudi nyuma kwa watu, kutokea kwa manabii na makristo wa uongo, tangazo la mpingakristo kwamba ni Mungu, na kutiwa giza jua na mwezi pamoja na kuanguka kwa nyota, wakati karibu na kurudi Kwake.
Walakini kwa habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake (Mathayo 24:36).Mara nyingi andiko hili linatajwa kinyume cha mantiki yake! Kwa kawaida linatajwa ili kuunga mkono dhana kwamba hatuna habari Yesu atarudi lini, kwa sababu anaweza kurudi wakati wowote na kunyakua kanisa. Lakini katika mantiki yake, Yesu hakumaanisha hicho. Alikuwa ndiyo kamaliza kuhakikisha kwamba wanafunzi Wake wangekuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake kwa kuwaambia ishara nyingi ambazo zingetokea muda mfupi tu kabla ya kurudi Kwake. Sasa anachowaambia ni kwamba, siku hasa na saa havitafunuliwa kwao. Tena, Yesu hasemi juu ya kuja Kwake mara ya kwanza kabla ya kipindi cha Dhiki ya miaka saba kuanza, wakati ambapo kanisa lingenyakuliwa, bali kuhusu kurudi Kwake wakati wa mwisho au karibia mwisho wa Dhiki. Hilo halina matatizo ukitazama mantiki vizuri.
Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile ziliozkuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.[9] Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja (Mathayo 24:37-44).Hapa tena, kitu ambacho Yesu anajali ni kwamba wanafunzi Wake wawe tayari kwa ajili ya kurudi Kwake. Hicho ndicho kilisababisha yote aliyosema kabla ya hapa na baada ya hapa, katika mafundisho Yake.Maonyo Yake mwengi kwamba wawe tayari na wakeshe si kwamba ni kwa kuwa kurudi Kwake kutakuwa kwa kushtukiza, bali ni ishara ya jinsi ambavyo itakuwa vigumu kwa sababu ya upinzani wa wakati wenyewe, kuendelea kuwa macho na kuwa tayari. Basi, wale wanaotarajia Unyakuo kabla ya Dhiki, wakati wowote, wanaodhani kwamba wako tayari kuliko Wakristo wengine, wanaweza wasiwe tayari kwa uhalisi kabisa, kwa kile kinachokuja. Kama hawatazamii dhiki yoyote na wajikute katikati ya mateso ya dunia nzima, wakati wa utawala wa mpingakristo, jaribu la kuanguka linaweza kuwazidi nguvu. Afadhali kuwa tayari kwa kile kinachofundishwa na Maandiko kwamba kitatokea.
Muda wa majuma sabini [bila shaka ni majuma yanayowakilisha miaka kama tutakavyoona – jumla ya miaka 490] umeamriwa juu ya watu wako [Israeli], na juu ya mji wako mtakatifu [Yerusalemu], ili kukomesha makosa [labda maana yake ni tendo kuu la dhambi kwa Israeli – kumsulubisha Masiya wao], na kuishiliza dhambi [pengine maana yake ni kazi ya ukombozi ya Kristo pale msalabani], na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu [maana yake ni ile kazi ya Kristo ya ukombozi pale msalabani], na kuleta haki ya milele [mwanzo wa utawala wa Yesu duniani], na kutia muhuri maono na unabii [pengine kuonyesha mwisho wa kuandikwa kwa Maandiko Matakatifu, au kutimizwa kwa unabii wote unaohusiana na utawala wa Miaka elfu], na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu [pengine kusimamishwa kwa hekalu la kipindi cha utawala wa Kristo miaka elfu moja hapa duniani]. Basi ujue na kufahamu ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu [amri hii ilitolewa na Mfalme Artashasta mwaka wa 445 K.K.] hata zamani zake masihi aliye mkuu [Bwana Yesu Kristo]; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili [yaani, jumla ya majuma 69 au miaka 483] utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu [hii inahusu kujengwa upya kwa Yerusalemu, uliokuwa umeharibiwa na WaBabeli]. Na baada ya yale majuma sitini na mawili [yaani, miaka 483 baada ya amri ya mwaka wa 445 K.K.], masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu [Yesu angesulubiwa mwaka wa 32B.K., tukihesabu mwaka kulingana na kalenda ya Kiyahudi yenye siku 360 kwa mwaka]; na watu [Warumi] wa mkuu atakayekuja [mpingakristo] watauangamiza mji na patakatifu [maelezo kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu mwaka wa 70 B.K. na majeshi ya Kirumi chini ya uongozi wa Tito]; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Naye [huyo ‘mkuu atakayekuja’ – mpingakristo] atafanya agano thabiti na watu wengi [Israeli] kwa muda wa juma moja [au miaka saba – hiki ni kipindi cha Dhiki]; na kwa nusu ya juma hiyo [yaani, miaka mitatu na nusu] ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu [wakati mpingakristo atakapojisimamisha mwenyewe katika hekalu la Kiyahudi huko Yerusalemu na kujiita Mungu – ona 2Wathes. 2:1-4]; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu [Yesu atakuja, na kumshinda mpingakristo] (Danieli 9:24-27. Maneno mepesi kukazia).
Wakati huo Mikaeli [malaika] atasimama, jemadari mkuu asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo [bila shaka hii ni ile dhiki ambayo Yesu alisema juu yake katika Mathayo 24:21]; na wakati huo watu wako wataokolewa [pengine ndiyo kule kukimbia kwa Wayahudi, au kuokolewa kwa waamini wakati wa Unyakuo]; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele [huu ni ufufuo wa wenye haki na waovu]. Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele. [Baada ya ufufuo wao, wenye hai watapokea miili mipya itakayong’aa kwa utukufu wa Mungu.] Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. [Maendeleo ya kushangaza sana katika usafirishaji na maarifa katika karne iliyopita yanaonekana kutimiza unabii huu.]
Ndipo mimi, Danieli, nikatazama, na kumbe, wamesimama wengine wawili, mmoja ukingoni mwa mto upande huu, na mmoja ukingoni mwa mto upande wa pili. Na mmoja akamwuliza yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto; ‘Je! Itakuwa muda wa miaka mingapi hata mwisho wa mambo haya ya ajabu?’ Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji yam to, hapo alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kueloekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati [sawa na miaka mitatu na nusu, kulingana na ufunuo wenye kufumbua katika Ufunuo 12:6 na 12:14); tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa. [Sawa tu na jinsi Danieli 7:25 ilivyotueleza kwamba watakatifu watatiwa mikononi mwa mpingakristo kwa miaka mitatu na nusu. Inaonekana dhahiri kwamba ni ile miaka mitatu na nusu ya mwisho katika ile miaka saba ya Dhiki. Mwisho wa matukio hayo yote yaliyotajwa na malaika utakuja wakati “nguvu za watakatifu” zitakapokwisha “kuvunjwa.”] Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, ‘Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?’ Akasema, ‘Enenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho. Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika [kwa njia ya dhiki bila shaka]; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndiyo watakaoelewa. Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini. [Hizo siku zisitafsiriwe kumaanisha muda utakaopita katikati ya hayo matukio mawili, kwa sababu yote yanatokea katikati ya ile miaka saba. Inatakiwa kueleweka hivi: tangu wakati wa matukio hayo mawili, siku 1,290 zitapitampaka kitu kingine kikubwa kitakapotokea mwishoni. Siku 1290 ni zaidi ya miaka mitatu na nusu kwa siku 30, kwa hesabu ya miaka yenye siku 360. Muda huu hutajwa mara kwa mara katika maandiko ya kinabii ya Danieli na Ufunuo. Sababu ya kuongezwa hizo siku thelathini haitajwi na haijulikani. Tena, malaika akamwambia Danieli hivi:] Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano. [Sasa tena tuna siku zingine arobaini na tano zisizojulikana ni za nini.] Lakini enenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utasimama [kufufuka kwa Danieli mwenyewe] katika kura yako mwisho wa siku hizo. (Danieli 12:1-13).Ni dhahiri kwamba kitu kizuri sana kitatokea mwisho wa hizo siku 75 za ziada! Itabidi tusubiri ili tuone.
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa … Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake, kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki, tangu sasa na hata milele (Isaya 9:6, 7. Manenomepesi kukazia).Vivyo hivyo, malaika Gabrieli alimtangazia Mariamu kwamba Mtoto wake angetawala ufalme usio na mwisho. Alimwambia hivi:
Malaika akamwambia, ‘Usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho’ (Luka 1:30-33. Maneno mepesi kukazia).[12]Wakati wa Miaka Elfu, Yesu binafsi atatawala kutoka Yerusalemu, pale Mlima Sayuni, na mlima huo utainuliwa na kuwa mrefu kuliko sasa. Utaala Wake utakuwa wa haki kabisa kwa mataifa yote, na itakuwepo amani kamili na halisi duniani kote.
Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, ‘Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake. Maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upana juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe (Isaya 2:2-4).Hata Zekaria naye alitabiri hayo hayo, kama ifuatavyo:
BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Mimi nina wivu kwa ajili ya Sayuni, wivu mkuu, nami nina wivu kwa ajili yake kwa ghadhabu kuu.’ BWANA asema hivi, ‘Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji wa kweli; na Mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa, Mlima Mtakatifu.’ … BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Itatokea halafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa miji mingi; wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, ‘Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za BWANA, na kumtafuta BWANA wa majeshi; mimi nami nitakwenda.’ Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA wa majeshi, na kuomba fadhili za BWANA. BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naama, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi’. (Zekaria 8:2-3; 20-23).Biblia inafundisha kwamba waamini watatawala pamoja na Kristo katika kipindi hicho cha miaka elfu moja. Viwango vya majukumu na wajibu zao katika ufalme Wake vitategemeana na uaminifu wao kwa sasa (ona Danieli 7:27; Luka 19:12-27; 1Wakor. 6:1-3; Ufunuo 2:26, 27; 5:9, 10 na 22:3-5).
Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa. … Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema BWANA (Isaya 65:19, 20, 25. Ona pia Isaya 11:6-9).Biblia imetaja sana habari za Miaka Elfu inayokuja – hasa katika Agano la Kale. Ukitaka kujifunza zaidi, soma Isaya 11:6-16; 25:1-12; 35:1-10; Yeremia 23:1-5; Yoeli 2:30 hadi 3:21; Amosi 9:11-15; Mika 4:1-7; Sefania 3:14-20; Zekaria 14:9-21 na Ufunuo 20:1-6.
Bwana ndiye aliye mkuu, na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, katika mlima wake mtakatifu. Kuinuka kwake ni mzuri sana, ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu. Mungu katika majumba yake amejijulisha kuwa ngome.Maana, tazama, wafalme walikusanyika; walipita wote pamoja. Waliona, mara wakashangaa; wakafadhaika na kukimbia. Papo hapo tetemeko liliwashika, utungu kama wa mwanamke azaaye (Zaburi 48:1-6. Maneno mepesi kukazia).Wakati Yesu atakaposimamisha utawala Wake huko Yerusalemu wakati wa kuanza kwa kipindi cha Miaka Elfu Moja, inaonekana kwamba watawala wengi wa dunia watakaopona Dhiki watapata taarifa ya utawala wa Yesu na kusafiri kwenda huko ili kujionea wenyewe! Watakachokiona kitawashangaza.[13]
Hapo ndipo mwisho, [Yesu] atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. Kwa kuwa, ‘Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake’ [Zaburi 8:6]. Lakini atakaposema, ‘Vyote vimetiishwa,’ ni dhahiri ya kuwa yeye [Baba] aliyemtiishia vitu vyote hayumo. Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake [Baba], ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.Shetani ambaye atakuwa amefungwa kwa kipindi chote hicho cha miaka elfu, atafunguliwa mwisho wake. Ndipo atawadanganya wale ambao ndani yao wanamwasi Yesu, waliokuwa wanajifanya kumtii wakati wa kipindi hicho chote (ona Zaburi 66:3).
Mbona mataifa wanafanya ghasia, na makabila wanatafakari ubatili? Wafalme wa dunia wanajipanga, na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu ya BWANA, na juu ya masihi wake [Kristo], ‘Na tuvipasue vifungo vyao, na kuzitupia mbali nasi kamba zao!’ Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake. ‘Nami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.’ [Yesu sasa anazungumza na kusema hivi:] ‘Nitaihubiri amri. BWANA aliniambia, Ndiwe mwanangu, mimi leo nimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.’ Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe. Mtumikieni BWANA kwa kicho, shangilieni kwa kutetemeka. Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira nanyi mkapotea njiani, kwa kuwa hasira yake itawaka upesi. Heri wote wanaomkimbilia!
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi. Katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake (2Petro 3:10-14. Ona pia Isaya 65:17, 18).Hatimaye – Yerusalemu mpya utashuka kutoka mbinguni mpaka chini duniani (ona Ufunuo 21:1, 2). Mawazo yetu hayawezi hata kuanza kuelewa utukufu wa mji huo, wenye eneo kubwa sana – karibu nusu ya bara la Afrika (ona Ufunuo 21:16), au maajabu ya miaka hiyo isiyo na mwisho. Tutaishi katika jamii kamilifu milele, chini ya utawala wa Mungu, kwa utukufu wa Yesu Kristo!